• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Malinyi District Council
Malinyi District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/Asili
      • Ukubwa wa Eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya Viongozi
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Maji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • kilimo, umwagiliaji na ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
      • Mipango
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ufugaji wa Nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Machine Investment
    • Skimu ya Umwagiliaji
  • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili Madiwani
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Kata
      • Biro
      • Igawa
      • Itete
      • Kilosa Mpepo
      • Mtimbira
      • Malinyi
      • Njiwa
      • Ngoheranga
      • Sofi
      • Usangule
    • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Matamko ya mbalimbali
    • Taarifa kwa Umma
    • Maktaba ya Video

WAHE. MADIWANI WATAKIWA KUWA MFANO WA KUTOA HAMASA KUEKEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NOVEMBA 27, 2024

Posted on: October 30th, 2024

Wahe. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi wametakiwa kuwa mfano wa kutoa hamasa kwa Wananchi kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27, 2024 ili Wananchi waweze kujitokeza kwa wingi kuchagua Viongozi wanaowataka na kuhakikisha Uchaguzi unafanyika kwa haki, Amani na utulivu.


Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Malinyi Bi Saida Mhanga wakati akitoa neno la Serikali kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba katika baraza la kawaida la Madiwani lililofanyika leo Oktoba 30 kwa ajili ya kujadali taarifa za utekelezaji robo ya kwanza Julai- Septemba katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.


Bi Saida Mhanga pia amewataka Viongozi na timu ya Wataalamu kutoka Halmashauri kuhakikisha miradi yote Serikali inayotekelezwa Malinyi inatekelezwa kwa wakati, kwa ubora na kuongeza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo uendane na thamani ya pesa amabazo Serikali inagharamia ili kusogeza huduma karibu zaidi na Wananchi.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mhe. Pius Mwelase ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ngoheranga amewaomba Wahe. Madiwani kusimamia vyanzo vya makusanyo vya mapato katika maeneo yao ili Halmashauri iweze kukusanya kwa Wingi na kukamilisha miradi iliyokusudiwa kutekelezwa kwa mwaka huu 2024/2025.


Aidha Mhe. Mwelase amesema kuwa mara baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kumalizika Halmashauri inatarajia kuendesha semina elekezi kwa Watendaji ngazi ya Vijiji ili kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu.


Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Khamis Jaaphar Katimba amesema Malinyi inaendelea vizuri ambapo mpaka mwezi kufikia Oktoba 2024 Halmashauri imekusanya kwa asilimia 60, na kuongeza kuwa asilimia 40 ya makusanyo hayo inakwenda katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.


Sambamba na hilo Ndugu Katimba amewashukuru Wajumbe wa Baraza la madiwani kwa kuzingatia mafunzo ya utawala Bora aliyoyatoa mwezi Septemba ambapo mafunzo hayo yamewezesha Mkutano huu wa Baraza la Madiwani kwa mara ya Kwanza kufanyika chini ya dakika 30 na kuwaomba Wajumbe hao ushirikiano Zaidi katika kutekeleza majukumu mengine ya Serikali.


Hata hivyo Mjumbe wa Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Itete Mhe. Anatory Libawa amesema Wahe. Madiwani kwa pamoja wamekubaliana kupunguza ushuru wa pumba kutoka sh. 1500 hadi sh 500 ili kutoa nafasi kwa Wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali kuja Malinyi kununua pumba kwa wingi Zaidi.

 

Matangazo

  • No records found
  • Angalia yote

Habari za hivi punde

  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA MALINYI ATOA WITO KWA WAKAZI WA MALINYI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA NA KUHAKIKI TAARIFA ZAO

    May 16, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MALINYI AWATAKA WATENDAJI KATA NA VIJIJI KUHAKIKISHA WANAFUNZI WOTE WANAPATA CHAKULA CHA MCHANA SHULENI

    May 15, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MALINYI AWATAKA WATENDAJI KATA NA VIJIJI KUHAKIKISHA WANAFUNZI WOTE WANAPATA CHAKULA CHA MCHANA SHUKENI

    May 15, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI JIMBO LA MALINYI KHAMIS KATIMBA AFUNGUA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA JIMBO LA MALINYI AWMU YA PILI

    May 14, 2025
  • Angalia yote

Video

DAS MALINYI AKIKABIDHI PIKIPIKI KWA WARATIBU ELIMU KATA
Video zaidi

Tovuti za haraka

  • Matangazo
  • Habari za Hivi punde

Tovuti Mashuhuri

  • Tamisemi
  • Tovuti ya Ajira
  • Matokeo ya Darasa la Saba 2022
  • Matokeo ya Kidato cha Nne
  • SALARY SLIP PORTAL
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2018

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi

    Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro

    Telephone: 0643111999

    Mobile:

    Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.