Katika kusherehekea siku ya wanawake Duniani machi 8,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndg. Hawa L Mpossi ametumia nafasi hiyo jumapili tarehe 1 machi kuzungumza na wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Kipingo. Mkurugenzi amewaasa wanafunzi hao kuacha kabisa kujihusisha na mahusiano wakiwa wanafunzi hivyo siku zote wajue kusema" HAPANA"
Amewahimiza wanafunzi hao kuzingatia masomo yao zaidi kwa kusoma kwa bidii ili waweze kufikia ndoto zao na kuwa viongozi bora wa baadae, vilevile wawe na ujasiri ili kupambana na vishawishi ambavyo vinaweza kusitisha ndoto za maisha yao kwa kupata mimba wakiwa shuleni hivyo kukatisha masomo yao.
Baadae mkurugenzi aligawa taulo za kike pamoja na sabuni ya unga kwa wanafunzi hao.
OFISI ZINAPATIKANA ENDEO LA MISEGESE
Postal Address: P.O.BOX 18 Malinyi
Telephone: 0784502410
Mobile: 0755388218
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Hatimiliki©2017 MALINYIDC Haki zote zimehifadhiwa